STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 25, 2014

Ruvu Shooting yaanza tambo kisha Betram Mwombeki

KLABU ya Ruvu Shooting imetamba kuwa imelamba dume kwa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba, Betram Mwombeki na kudai timu pinzania zijiandae kukabiliana naye kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui ya Shinyanga.
Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire amesema kuwa kwa mara ya kwanza amemuona Mwombeki akiichezea Ruvu Shooting na kubaini kuwa ni mchezaji ambaye atawasaidia mno, baada ya kutoa pasi ya bao la kwanza na kufunga bao la pili timu hiyo ilipotoka sare ya mabao 2-2 na Mwadui kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani siku ya Jumatatu.
"Nashangaa kuna timu zilimuona hafai, huyu Mwombeki amecheza kwa kiwango cha hali ya juu, ametoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Abdurahman Mussa na kutufungia bao la pili, kwa kweli huyu ameziba kabisa pengo la Elius Maguri," alisema Masau.
Amezitahadharisha timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu kuwa zitakutana na moto wa Mombeki, kwani amerejea kwenye kiwango chake cha kawaida, akicheza kwa kutumia nguvu kama kawaida yake na kuachia mashuti makali.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, alisajiliwa na Ruvu kwenye kipindi hiki cha dirisha dogo kwa ajili ya kuziba pengo la Maguri ambaye kwa sasa yuko Simba.
Mwombeki alivuma akiwa na Simba msimu uliopita chini ya kocha Abdallah Kibadeni, lakini hali ilikuwa ngumu kwake alipokuja kocha matata Zdravko Logarusic ambaye hakupendezwa na aina yake ya uchezaji, kiasi cha kumtupia virago.
Ruvu ambayo itaanza kibarua cha ngwe nyingine ya Ligi Kuu kwa kuumana na ndugu zao Ruvu Shooting siku ya Jumamosi, imewasajili pia wachezaji wengine akiwamo Yahya Tumbo nyota wa zamani wa Africans Lyon na Yanga.

No comments:

Post a Comment