STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 19, 2015

Hassan Dalali ajivunia rekodi yake Msimbazi

Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali
Hassan Dalali akisalimiana na wachezaji wa Bongo Movie siku ya Simba day
MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesema yapo mambo matano ambayo anajivunia kuiongoza klabu hiyo na jambo moja linamtia simanzi mpaka sasa kwa kuona hakufanikiwa kutekeleza.
Akizungumza na MICHARAZO, Dalali aliyataja mambo anayojivunia kwa kuiongoza Simba kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2008-2010 ni kuanzisha Simba Day mwaka 2009 ambayo inaendelezwa mpaka sasa na viongozi waliomfuata.
"Kuipatia Simba kiwanja kule Bunju ni suala jingine, kuwaunganisha wanachama wote wa Simba na kuongea idadi yao ni mambo mengine yanayonipa faraja," anasema.
Mwenyekiti huyo ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye masuala ya kisiasa akiwa Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Kinondoni na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa Wilaya ya Kinondoni alisema kubwa la kujivunia ni kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu bila kufungwa hata mchezo mmoja msimu wa 2009-2010.
"Hili linanifanya nitembee kifua mbele na kujivunia, kuifanya Simba isifunguke, tukishinda mechi 18 kati ya 20 na mbili tukitoka sare, Azam walijitahidi msimu wa 2013-2014, lakini hawakufikia rekodi kwani walishinda mechi 18 na kutoka sare 8, japo tulitofautiana idadi ya michezo, wao walicheza mechi 26 sisi 22," alisema Dalali.
Kuhusu linalomtia simanzi ni kitendo cha kushindwa kufanikisha ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo, na kitendo cha viongozi wenzake kushindwa kuuendeleza ingawa alimfagilia Ismail Aden Rage kwa kuweza kupunguza deni lililokuwapo kujimilikisha kiwanja hicho.
"Naamini kwa namna mimi na Mwina Kaduguda tulipokuwa tumefikia, hivi sasa Simba ingekuwa na eneo la kujivunia la kufanyia mazoezi yao kwa kujinafasi kwani tulikuwa tumeingia mkataba na kampuni ya kuuza jezi ya Marekani, ambapo hata hivyo ilisitisha."
"Ila naamini Simba itakuja kuwa na Uwanja wake na kama nitakufa basi wanachama wa Simba watanikumbuka kwa mambo hayo,  ya kiwanja na tamasha la Simba Day," alisema Dalali.

No comments:

Post a Comment