
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti la Marca, zimedai kuwa taratibu zote za Pedro kujiunga na Chelsea zimeshakamilika baada ya klabu hizo kuafikiana uhamisho wa Euro Mil. 28, huku kukiwa na nyongeza ya Euro Mil. 2 itakayolipwa baadaye. Taarifa hizo ziliendelea kudai kuwa Pedro tayari ameshatua jijini London kufanyiwa vipimo vya Afya baada ya kupewa ruhusa na Barcelona. Mashetani Wekundu, Man United ilikuwa wakitajwa kwa wiki kadhaa kumuwania mshambuliaji huyo kwa kutoa ofa ya Euro milioni 25.
No comments:
Post a Comment