STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 19, 2015

Kocha Man City aanza kuchonga mapema

http://s.ndtvimg.com/images/content/2015/aug/806/pellegrini-smile-man-city-chelsea-win.jpgUSHINDI una raha bhana we acha tu!, Meneja wa vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester City, Manuel Pellegrini ameanza kuchonga baada ya chama lake kupata ushindi katika mechi mbili mfululizo.
Kocha huyo ambaye ameiongoza Man City kuitoa nishai mabingwa watetezi, Chelsea, wikiendi iliyopita amesema wachezaji wake wana njaa na kiu baada ya kulikosa taji la Ligi Kuu msimu uliopita. 
City walimaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya mabingwa Chelsea wakitofautiana kwa alama nane. 
Akihojiwa mara baada ya kikosi chake kuichapa Chelsea kwa mabao 3-0 jana, Pellegrini amesema pengine kilichotokea msimu uliopita kilikuwa ni uzoefu tosha kwao. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wachezaji wake hivi sasa wana njaa na kiu ndio maana wanataka kushinda katika kila mchezo. 
Mabao ya City katika mchezo huo yalifungwa na Sergio Aguero, nahodha Vincent Kompany na Fernandinho.
Kikosi hicho kinatarajiwa kushuka dimbani wikiendi hii ugenini kuvaana na Everton siku ya Jumapili.

No comments:

Post a Comment