STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 15, 2016

CUF na sitaki nataka yao kwa Prof Lipumba

https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/6/69/Ibrahim_Lipumba.jpg
Prof Lipumba
CHAMA cha Wananchi CUF, kimetoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyonukuliwa ni ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shaarif Hamad kwamba, aliyekuwa Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Harun Lipumba akautafute uenyekiti mahali penmgine na sio kwenye chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa ilitolewa na Idara ya Habari ya Chama hicho na kusainiwa na Mkurugezi wake, Saluim Bimani ni kwamba kilichoripotiwa na vyombo vya habari ni propaganda za kuivuruga CUF.
Taarifa yake rasmi inasomeka ka ilivyo hapo chini, ikiwa ni siku chache baada ya Prof Lipumba kudai atawania nafasi ya Uenyekiti katika uchaguzi wa CUF ikiwa ni miezi kadhaa tangu alipotangaza kujiuzulu mara baada ya Ukawa kumteua Edward Lowassa kuwa Mgombea Urais wa umoja huo unaojumuisha vyama vya Chadema, NLD, NCCR Mageuzi na CUF.
http://www.jamiiforums.com/attachments/index-jpeg.356758/

No comments:

Post a Comment