![]() |
| Picha tofauti zikionyesha basi la tahmeed lilivyougua moto na kuteketea kabisa |
SIMANZI. Habari zilizotufikia muda huu zinasema kuwa, basi la Tahmeed linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga limeungua lote kwa moto mapema leo katika kijiji cha Komkoma.Jambo la kushukuru kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba hakuna abiria yeyote miongoni mwa waliokuwa katika basi hilo ambao wamejeruhiwa.
Hata hivyo ni kwamba abiria wamepata hasara baada ya mizigo yao kuteketea kwa moto huo uliozuka ghafla eneo la nyuma kutokana na kile kilichoelezwa hitilafu ya umeme ndani ya gari hilo, ingawa wahusika hawakufafanua chanzo halisi cha moto.

No comments:
Post a Comment