STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 15, 2016

Dunga adunguliwa kweupe Brazili

http://bloximages.newyork1.vip.townnews.com/gwinnettdailypost.com/content/tncms/assets/v3/editorial/0/09/009efebc-e732-51ed-8601-b018f1f571c8/5760a8c0cc0e4.image.jpg
Dunga aliyedunguliwa Brazili
HAWAREMBI! Shirikisho la Soka la Brazil, limeamua kumfuta kazi kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Dunga baada ya kutolewa katika hatua za awali za michuano ya Copa America inayoendelea nchini Marekani.
Nahodha huyo wa zamani wa kikosi cha Brazil kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 1994, aliteuliwa kuwa kocha wa timu hiyo kwa mara ya pili mwaka 2014.
Lakini majuzi timu yake iling’olewa katika hatua ya makundi ya Copa America kwa mara ya kwanza toka mwaka 1987 kufuatia kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Peru katika mchezo uliofanyika huko Massachusetts Jumapili iliyopita.
Dunga mwenye umri wa miaka 52, aliwahi kuinoa Brazil mwaka 2006 mpaka 2010 na kufanikiwa kushinda taji la Copa America mwaka 2007. Kocha wa klabu ya Corinthians, Tite ndio anayepewa nafasi kubwa ya kutwaa mikoba ya Dunga.

No comments:

Post a Comment