STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 13, 2013

AZAM YATETEA TAJI LAKE LA KOMBE LA MAPINDUZI ZANZIBAR

Mgeni rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Mapinduzi, Nahodha wa Azam FC, Himid Mao Mkami usiku wa jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya timu hiyo kutwaa taji hilo kwa kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1 ndani ya dakika 120.

Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akigombea mpira na beki wa Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 
Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akimtoka mpira na beki wa Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 

Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akikimbia na mpira dhidi ya beki wa Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 
Mwaikimba akifumua shuti
Mshambuliaji wa Azam FC, Seif Abdallah akimiliki mpira mbele ya beki wa Tusker FC, Bright Jeremiah katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 
Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akimtoka beki wa beki wa Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 
Shuti la bao, Mwaikimba akiwa amefumua shuti kuifungia Azam bao la ushindi
Wachezaji majeruhi wa Azam, John Bocco 'Adebayor' kushoto na Abdulhalim Humud 'Gaucho' kulia wakiingia uwanjani
Mpira uko nyavuni, mkwaju wa Penalti wa Joackins Atudo umetinga kimiani kuipatia Azam bao la kusawazisha huku kipa Samuel Odhiambo akigagaa chini 
Hongera shujaa Mwaikimba, wachezaji wa Azam wakimpongeza mfungaji wa bao lao la ushindi
Kikosi cha ubingwa jana
Washindi wa pili Tusker FC kikosi chao cha jana
Nahodha Himi Mao akiinua juu burungutu la fedha, Sh. Milioni 10 za ubingwa 
Mgeni rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akimkabidhi donge nono la Sh. 300,000 mfungaji bora wa Kombe la Mapinduzi, Jesse Were wa Tusker FC aliyemaliza na mabao matano usiku wa jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Binti aliyevamia uwanjani dakika ya 89 akitolewa nje na askari Polisi

Mgeni rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akimkabidhi Kombe la ushindi wa pili wa Mapinduzi, Nahodha wa Tusker FC, Joseph Shikokoti usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Polisi wakimtoa nje binti aliyevamia uwanjani dakika ya 89

Azam wakisherehekea na Kombe lao

Mwaikimba akifuaria na mashabiki Kombe lililotokana na juhudi zake 
Azam wakisherehekea na Kombe lao
Brian Umony wa Azam amemuacha chini Joseph Shikokoti wa Tusker FC
Umony na Shikokoti
Mwaikimba aliyeruka hewani kuiga kichwa kwenye lango la Tusker kufuatia mpira wa kona
Mwaikimba mawindoni


Refa akijaribu kumzuia binti wakati anakatiza uwanjani
Mwaikimba mbele ya Shikokoti

Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
AZAM FC wamefanikiwa kutetea Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1.
Kwa ushindi huo, Azam wamezawadiwa Sh. Milioni 10, wakati washindi wa pili Tusker wamepata Sh. Milioni 5.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ramadhan Rajab Ibada ‘Kibo’ aliyesaidiwa na Mwanahija Makame Mfumo na Mgaza Kindundi, hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.
Azam ndio walioshambulia zaidi katika kipindi hicho, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga bao japo moja. Gaudence Mwaikimba alipewa pasi nzuri na Brian Umony dakika ya 44, lakini shuti lake kali lilidakwa na kipa Samuel Odhiambo.
Kipindi cha pili, Tusker walirudi na moto mkali na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Azam.
Hiyo iliwasaidia mabingwa hao wa Kenya kupata bao dakika ya 60, lililofungwa na Jesse Were aliyeunganisha kwa shuti kali la kimo cha mbuzi pasi ya Robert Omunok.
Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha dakika ya 72 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na beki Mkenya, Joackins Atudo baada ya beki wa Tusker, Luke Ochieng kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Katika dakika mbili za nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 90 za mchezo huo, alijitokeza binti mwenye umri kati ya 14 na 16 na kukatiza uwanjani akitokea jukwaa la Urusi.
Refa alijaribu kumsimamisha, lakini aliendelea kukatiza Uwanja hadi nje ambako alipokewa na askari Polisi na kutolewa nje kabisa ya Uwanja. Mtangazaji wa Uwanja wa Amaan, Farouk Karim aliwatuliza mashabiki akisema binti huyo ametoroka hospitali ya vichaa, Kidongo Chekundu na tayari Polisi wamemkamata na kumrejesha huko.
Hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30.
Gaudence Exavery Mwaikimba aliipatia Azam bao la ushindi dakika ya pili tu tangu kuanza kwa muda wa nyongeza baada ya kuwazidi nguvu na maarifa mabeki wa Tusker.
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Humphrey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Brian Umony/Malika Ndeule dk126 na Uhuru Suleiman/Seif Abdallah dk64.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Bright Jeremiah, Martin Kizza, Joseph Shikokoti, Frederick Onyango/Mark Ochiambo dk93, Andrew Tolowa/Edwin Ombasa dk 55, Khalid Aucho/Benson Amianda dk 80, Jesse Were/Andrew Sekayambya dk54, Ismail Dunga/Michael Olunga dk52 na Robert Omunok.
 
KWA HISANI YA BIN ZUBEIRY 

No comments:

Post a Comment