| Mlezi wa timu ya Goldoen Bush Veterani, Onesmo Waziri 'Ticotico' akihojiwa na waandishi wa habari katika mchezo wao na Wahenga Fc ambapo timu yao ilishinda mabao 4-3. |
| Mshambuliaji Herry Morris akitafakari wakati wa mapumziki, ambapo alishatupia mabao mawili na kuisaidia Golden Bush kushinda mabao 4-3. |
| Wachezaji wa Golden Bush Veterani wakiwa mapumziko |
| Herry Morris akihojiwa na waandishi |
| Beki wa timu ya Golden Bush, Majaliwa 'Afande' akijohiwa pia kwenye mchezo huo |
| Yona Babadimo wa Wahenga Fc naye akihojiwa wakati timu yake ikichezea kipigo toka kwa Golden Bush jana jijini Dar es Salaam waliposherehekea Mapinduzi na kuukaribisha mwaka 2013 |
| Mengi Matunda mchezaji wa Wahenga akijohiwa baada ya kupumzishwa na benchi lake la ufundi |
| Said Swedi 'Panucci' akikokota mpira katika pambano lao la jana |
| Njoo sasa! Ndivyo anayoelekea kusema beki wa Wahenga 'Mohammed huku Godfrey Katepa wa Golden Bush akimfuata |
| Achia wewe! Said Swedi (3) akichunana na mchezaji wa Wahenga katika pambano lao la jana |
| Kama Ronaldo! Mchezaji wa Wahenga akijiandaa kupiga mpira huku Shaaban Kisiga (19) wa Golden Bush akimfuatilia sambamba na wachezaji wenzake |
| Mimi ndio Macocha! Macocha Mayay wa Wahenga akimtoka Godfrey Katepa (kulia) huku akichungwa na Salum Swedi 'Kussi' wa Golden Bush Veterani. |
| Wachezaji wa Wahenga na Golden Bush wakiwajibika uwanjani timu zao zilipokutana jana na Golden Bush kushinda mabao 4-3 |
| Macocha wa Wahenga Fc akijaribu kutafuta mbinu za kumtoka Saidi Swedi wa Golden Bush |
| Mzee Hamis wa Wahenga akikokota mpira pembeni ya uwanja wa TP wakati timu yake ilipoumana na Golden Bush na kuchezea kichapo cha mabao 4-3 |
| Wazir Mahadhi (10) akichuana na wachezaji wa Wahenga wakati akiiongoza timu yake kulipa kisasi cha mabao 4-3 kwa wapinzani wao. |
| Pilikapilika uwanjani wakati Wahenga Fc na Golden Bush zilipomenyana jana jijini Dar es Salaam |
| Onesmo Waziri 'Ticotico' (4) akipongezwa na Athuman Machupa wakati wakimpisha uwanjani jana katika pambano lao dhidi ya Wahenga Fc. |
| Jamani Mpo Wapi! Beki wa Wahenga Fc akijiandaa kupiga mpira mbele |
| Mahadhi akichuana na mchezaji wa Wahenga katika mechi ya jana |
| Said Swedi 'Panucci' (3) akitafakari namna ya kuupiga mpira wakati wa pambano lao la Golden Bush dhidi ya Wahenga ambapo walifanikiwa kushinda mabao 4-3 |
| Macocha Mayay wa Wahenga (kulia) akiwatoka wachezaji wa Golden Bush, Shaaban Kisiga (kushoto) na Shija Katina (8) |
| Berki wa Wahenga Fc akihamisha mpira mbele ya Herry Morris (kulia) |
| Hapa Kazi Tu! |
| MTANIKOMA! Macocha akiwaacha wachezaji wa Golden Bush katika pambano la jana, mchezaji huyu ndiye aliyekuwa nyota kwa upande wa Wahenga, japo timu yake ililala kwa mabao 4-3 |

No comments:
Post a Comment