STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 9, 2013

Ramadhani Shauri kuwania taji la Dunia

Ramadhani Shauri


BINGWA wa Afrika anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Ngumi za Kulipwa la IBF, Ramadhani Shauri ameteuliwa kuwania ubingwa wa vijana wa dunia wa IBF.
Kwa mujibu wa taarifa ya IBF/USBA, inasema kuwa bingwa huyo wa uzito wa Feather atawania taji hilo la dunia katika uzito wa light kwa vijana chini ya umri wa miaka 25.
Shauri alitwaa taji hilo la Afrika kwa kumchapa Mganda, Sunday Kizito katika pambano laio lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ya IBF/USBA iliyotolewa na rais wa shirikisho hilo, Onesmo Ngowi ni kwamba hiyo ni fursa nzuri kwa Mtanzania huyo kuweza kujitangaza kimataifa iwapo atafanikiwa kutwaa taji hilo la dunia la vijana.
Inaelezwa IBF iliamua kumpatia Shauri nafasi ya kugombea ubingwa huo wa vijana baada ya kuangalia mkanda wa video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika na kuridhika kuwa anaweza kushindania ubingwa huo wa vijana,
Mabondia wengi wa Marekani waliokuja kuwa mabingwa wa dunia na kuweza kupata pesa nyingi walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana hivyo kuweza kupanda chati kwenye viwango vya IBF.
Mifano wa mabondia hao ni akina Bernard Hopkins, Floyd Maywealther na Oscar De la Hoya.
Iwapo Shauri atashinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana atakuwa kwenye macho ya mapromota wakubwa duniani kama kina Don King, Bob Arum na wengine wengi.
Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwa historia ya ngumi nchini kwa Mtanzania kutwaa taji kubwa kati ya manne duniani ya IBF, WBA, WBO na WBC.
Kadhalika inaeleza kushinda kwa Mtanzania huyo kutatoa fursa kwa nchi ya anzania kujitangaza kibiashara na utalii duniani.

No comments:

Post a Comment