STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 9, 2013

Baby Madaha afyatua mpya akijiandaa kwenda kuwania tuzo Nigeria



Baby Madaha katika pozi

WAKATI filamu yake ya 'Ray of Hope' ikiteuliwa kwenda kuwania tuzo ya kimaataifa za African Magic nchini Nigeria, msanii nyota nchini wa filamu na muziki, Baby Madaha anajiandaa kupakua filamu mpya   iitwayo 'Tatakoa'.
Akizungumza na MICHARAZO, Madaha alisema filamu hiyo imekamilika na ipo katika hatua za kuingizwa sokoni ikiwa imeshirikiana na wasanii kadhaa nyota nchini akiwamo Jumanne Kihangale 'Mr Tues'.
Madaha aliwataja wasanii wengine walioshiriki filamu hiyo inayozungumzia masuala ya mapenzi, uchawi na mauaji ni Salma Jabu 'Nisha', Frola Mvungi, Mariam Mndeme na wengineo.
"'Tatakoa' ni filamu ya aina yake imesheheni uchawi, mapenzi na mauaji ndani yake, yaani nimekuja kama Angelina Jolie," Baby Madaha alitamba.
Alisema wakati filamu hiyo ikiwa njiani, kazi yake iliyonyakua tuzo za ZIFF-2012 ya 'Ray of Hope' imeteuliwa kuwania tuzo za filamu za kimataifa za African Magic ambazo zitafanyika mwezi ujao nchini Nigeria.
Madaha alisema amefurahi kuona filamu hiyo ikiziangusha nyingine za wasanii wakongwe nchini na Afrika Mashariki katika mchujo wa kupenya kuwania tuzo hizo maarufu Afrika na duniani kwa ujumla.
Msanii alisema kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya safari hiyo ya kwenda Nigeria, akiwaomba Watanzania wamuombee aweze kuibuka kidedea katika tuzo hizo.

Baby Madaha katika pozi jingine matata

No comments:

Post a Comment