STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 9, 2013




SIMBA, OLJORO HAPATOSHI LEO ARUSHA, AZAM ZAMU YAO KESHO


LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 16 leo kwa mechi kadhaa ambapo jijini Arusha, mabingwa watetezi Simba itavaana na wenyeji wao JKT Oljoro.
Mechi hiyo namba 129 itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, huku Simba ikiingia na kumbukumbu ya sare katika mechi yake iliyopita dhidi ya JKT Ruvu wakati wenyeji wao wakiwa wameshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Simba italazimika kupata ushindi ili kufufua mbio zao za kuwania taji hilo kwa mara ya pili mfululizo ambalo linawindwa na timu za Yanga iliyopo kileleni na Azam wanaoshika nafasi ya pili ambao kesho watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar mjini Manungu, Morogoro.

Mechi nyingine zinazochezwa leo Jumamosi ni pamoja na kivumbi kitakachowaka uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, wakati wenyeji  Kagera Sugar na Mgambo Shooting zitaonyeshana kazi katika pambano litakaloamuliwa na mwamuzi Amon Paul kutoka Musoma, Mara.
Toto Africans baada ya kufanya vibaya katika mechi tatu zilizopita ugenini imerejea nyumbaji jijini Mwanza itakapoumana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo utaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor BinSlum, aliweka wazi kwamba huenda mchezaji wao wa kimataifa kutoka Brazil, Gabriel Barbosa, ambaye ITC yake imeshapatikana atashuka dimbani katika pambano hilo.
Mchezaji huyo alikwama karibu duru zima la msimu huu kuichezea Coastal kwa kukosa hati hiyo, lakini Binslum kaithibitishia MICHARAZO kwamba kila kitu sasa kipo shwari na wapo tayari kumtumia mchezaji wao huyo.
Mwamuzi Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani ndiye atakayechezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons na African Lyon ambayo imepata huduma za kocha mpya Salum Bausi kutoka Zanzibar. Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kwa Bausi kuiongoza timu katika VPL.
Maofisa wengine wa mechi hiyo ni mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Rashid, mwamuzi msaidizi namba mbili Abdallah Mkomwa wote kutoka Pwani wakati mwamuzi wa mezani ni John Kanyenye wa Mbeya. Kamishna wa mechi hiyo ni Rashid Rwena kutoka Ruvuma.
Mechi kati ya Mtibwa Sugar na Azam iliyokuwa ichezwe kesho imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo sasa itafanyika Jumapili katika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro.

Kikosi cha Azam

No comments:

Post a Comment