STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 2, 2013

Mwanamke ajipiga sindano 54 ili kukuza makalio yake











MWANAMKE mmoja nchini Marekani, ameeleza jinsi alivyonusurika kifo kufuatia hatua yake ya kuongeza makalio kwa kupiga sindano zenye kemikali mitaani.
Karmello mwenye umri wa miaka 23 kutoka mji wa Detroit, Michigan, anasema anasema amalizika kupiga sindano za kuongeza makalio 54 katika kipindi cha miaka mitatu ili kutimiza dhamira yake ya kuwa na mwili anaoutaka mwenyewe.
Anasema, kiasi cha sindano alichopiga ni sawa na lita kadhaa za maji, alitumia kiasi cha dola 15,000.
Kutokana na gharama kubwa ya kurekebisha mwili, Karmello alikuwa akifanya kazi hiyo kwa wataalamu wa mitaani, na kwamba alielezwa kama anahitaji zaidi kujenga makalio makubwa, apige sindano zingine 36.
Wakati wanawake wengine wamekuwa wakifanya hivyo kwa kufanyiwa upasuaji na kuongeza madini laini ya plastiki kwenye makalio, Karmello kwake ilikuwa tofauti kabisa, kwani yeye aliamua kupiga sindano.
Akieleza mkasa huo,  Karmello alisema kazi hiyo alikuwa akiifanya kupitia mtaalam mmoja mwanamke aliyekuwa akikutana naye kwenye hotel.
Karmello anasema ametumia kiasi kikubwa cha pesa kurekebisha makalio yake, na alikuwa akipata ushawishi zaidi kupitia kwa mwanadada mwingine aliyechanganyikia na kazi ya kuongeza makalio, Vanity Wonder.
Wonder, anadaiwa kutumia zaidi ya paundi 10,000 ili kujenga aina ya makalio aliyokuwa akiyataka.
Hata hivyo, dada huyo anasema alinusurikia kifo baada ya moja ya sindano aliyopiga kumpa maambukizo kwenye makalio.
Karmello anasema baada ya kuongeza makalio, aliamua kwenda kwa mtaalamu wa upasuaji wa kuongeza na kurekebisha mwili, Dr Anthony Youn, Karmello ambapo alimwambia hatari aliyonayo baada ya kuongeza makalio.
Uchunguzi wa Youn kupitia picha za  X-ray, zinaonyesha jinsi makalio ya mwanadada huyo yalivyo laini kama sponji na hiyo ni hatari kubwa kwake, kwani kama angepiga sindano zingine zingeweza kumsababishia kifo mara moja.
Karmello anaonye athari za kuongeza makalio kwa kutumia sindano akisema ni hatari sana.
“Kabla sijapiga sindano, makalio yangu yalikuwa saizi namba nne, lakini sasa niko kwenye saizi namba 10,” alisema mwanadada huyo.
“Nina furaha kwa sababu sikuwahi kuwa na makalio makubwa kama ilivyo sasa.
“Najisikia kama mwanamke aliyekamilika, mwenye umbo zuri na kuvutia. Kweli nina furaha kubwa kufanikisha hili.”
Mwanadada huyo anasema anajivunia kwa kiasi kikubwa umbo lake kwa sasa na jinsi anavyowateka watu wengi.
“Nimekuwa sehemu ya macho ya watu wengi kwa jinsi wanavyoniangalia kila nipitapo.
“Nimeweza kupata kile nilichokuwa nikihitaji katika maisha yangu kwa muda mrefu,’ alisema wakati akihojiwa katika kipindi maalum cha televisheni kinazungumzia maisha hali ya watu nchini Marekani
Kwa kawaida kazi ya kuongeza makalio hufanyika kwa kupiga sindano zenye silicon.
Karmella anasema alikuwa na rafiki yake, Vanity Wonder ambaye naye alikuwa kinara wa kuongeza makalio, na kuna wakati fulani ilibaki nusura apoteze maisha kutokana kuendekeza sana zoezi la kuongeza mwili.
Wakati wa kazi hiyo, Vanity hakujua kama anaweza kupata madhara makubwa kufuatia kuongeza mwili kupita kiasi mpaka alipopata tatizo kubwa lililotishia maisha yake.
Katika maelezo yake, Karmello alisema alikwenda kwa daktari na kumweleza dhamira yake ya kuongeza ukubwa wa makalio, na mtaalamu huyo alimweleza kwamba hilo ni jambo linalowezekana tena katika kipindi kifupi.


CHANZO:NIPASHE

No comments:

Post a Comment