STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 2, 2013

Azam waenda Sudan Kusini kumalizia kazi

MSAFARA wa watu 30 wakiwamo wachezaji 20 na viongozi 10 wa klabu ya Azam wameondoka nchini afajiri ya leo kuelekea Sudan Kusini kwa ajili ya kumalizia kazi katika pambano la marudiano la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao Al Nasir Juba.
Azam inatarajiwa kuvaana na Al Nasir kesho mjini Juba wakiwa na ushindi wa mabao 3-1 iliyopata katika mechi yao ya awali iliyochezwa nchini Tanzania wiki mbili zilizopita.Katibu Msaidizi wa Azam, Twalib 'Chuma' Suleiman, aliiambia MICHARAZO kikosi hicho kimeondoka alfajiri ya leo ikiwa na matumaini makubwa ya kwenda kuing'oa Al Nasir licha ya kukiri kwamba hawatadharau mchezo huo.
Chuma, alisema waliondoka katika msafara huo wa leo ni pamoja na wachezaji 20 wakiwamo makipa; Mwadini Ally na Aishi Manula, mabeki; Joackins Atudo, David Mwantika, Himid Mao, Malika Ndeule, Waziri Salum na Luckson Kakolaki.
Aliongeza wachezaji wengine ni viungo ni Kipre Balou, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Salum Abubakar, Humphrey Mieno, Abdi Kassim 'Babbi' na Khamis Mcha 'Vialli', huku washambuliaji wakiwa ni John Bocco 'Adebayor', Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Brian Umony na Gaudence Mwaikimba 'Caroll'. 

Kwa upande wa uongozi msafara huo umeambatana na Katibu Mkuu, Nassor Idrissa, ambaye anakuwa mkuu wa msafara, Mameneja, Patrick Kahemela, Jemedari Said, Ibrahim Shikanda na Abubakar Mapwisa.
Benchi la ufundi linaoongozwa na kocha mkuu, John Stewart Hall na wasaidizi wake, Kally Ongalla na Idd Abubakar, pia wamo Dardenne Paul na Yusuf Nzawila.

No comments:

Post a Comment