STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, June 8, 2013

Mfanyabiashara mbaroni kwa kulawiti wanafunzi


MFANYABIASHARA maarufu mjini Morogoro, Mohamed Mauji, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwaingilia kinyume na maumbile wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Mwere B.

Tukio hilo linadaiwa kutokea wiki iliyopita kwenye eneo la mazingira ya ofisi ya mfanyabiashara huyo anayeuza vinywaji laini kwa jumla.

Akizungumzia tukio hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro, Sadick Tindwa, alisema kuwa inadaiwa kutokea Mei 31 na kuripotiwa katika kituo hicho Juni 3 na wazazi wa watoto hao.

Alisema kuwa wazazi hao walieleza kuwa waliwabaini watoto wao baada ya kupewa taarifa na walimu wa shule hiyo kuwa watoto hao wamekuwa wakija shuleni na fedha nyingi za matumizi pamoja na vitu mbalimbali.

Mkuu huyo wa Polisi wilaya ya Morogoro alisema kuwa baada ya wazazi hao kupewa taarifa hizo, waliwauliza watoto hao na kueleza kuwa wamekuwa wakipewa na mtu waliyemtaja kwa jina la mzungu na kuwafanyia vitendo hivyo.

Alisema kuwa wazazi hao walipowapekua watoto wao waliwakuta wana michubuko katika sehemu za kutolea haja kubwa na kuamua kulifikisha suala hilo kwa afisa mtendaji wa kata Kingo jirani na mfanyabiashara huyo.

Mkuu huyo wa Polisi Wilaya ya Morogoro alisema kuwa afisa huyo mtendaji wa kata ya Kingo aliamuru suala hilo lifikishwe kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya kufanyiwa upelelezi.

Alisema kuwa baada ya kulifikisha , jeshi la polisi lilimkamata mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi ikiwa pamoja na watoto hao kupelekwa hospitali ya rufaa ya Morogoro kuchunguzwa afya zao.

Hata hivyo, alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na tuhuma hizo, mfanyabiashara huyo alikiri kuwafahamu wanafunzi hao ambao wamekuwa wakipita nje ya ofisi yake na kuomba pesa ya soda na yeye aliwahi kuwapatia kiasi cha sh 500 lakini hajawahi kuwafanyia kitendo hicho.

No comments:

Post a Comment