Naibu Waziri, Januari Makamba |
NAIBU Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema dhamira ya kuwepo
kwa vyama vingi bado haijafikiwa tangu kuanzishwa kwake kutokana na kukosa
vyama na viongozi wenye dira kwa Taifa.
Aliyasema hayo leo
jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanafunzi wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi ambao wanamaliza vyuo mbalimbali mkoa wa Dar es Salaam.
Makamba ambaye pia ni
Mlezi wa Vyuo Vikuu Tanzania alisema vyama
hivyo vimekuwa vikijikita katika kulalamika bila kuonyesha dira na mwelekeo
tofauti jambo ambalo linapelekea katika kufanya fujo ambazo zinakwamisha
jitihada za serikali.
Makamba alisema
Serikali inafanya kazi kutokana na mipango yake ambayo imejiwekea yenyewe hivyo
inaamini kuwa itafikia malengo yake bila kusukumwa na mtu.
“Kwa kweli najuta kwanini tuliruhusu uwepo wa
vyama vingi hapa nchini kwani lengo letu lilikuwa ni kudumisha demokrasia kitu
ambacho kimekuwa kinyume kwani vyama na
viongozi hao wamekuwa wakihubiri kinyume na dhima ya lengo husika,”
alisema
Naibu Waziri alisema
CCM ni chama ambacho kinaheshimika kitaifa na kimataifa hivyo wao wanaamini
kuwa heshima hiyo itaendelea kuwepo milele kwa milele.
Alisema vijana wa CCM
wahakikishe kuwa wanakisaidia chama na nchi kwa ujumla ili nchi isije kuchukuliwa na
vyama vya upinzani kwani itakuwa ni sawa na kuipeleka nchi kuzimu.
Aidha Mlezi huyo
aliwataka vijana hao wanaomaliza
kujiamini na kuthubutu kushiriki katika fursa mbalimbali zinazojitokeza ili waweze
kupata urahisi wa kushiriki katika chama na serikali kwani ni wajibu wao
kulitumikia Taifa.
Makamba alisema vijana
wanapaswa kushiriki katika harakati za kisiasa kwani hayupo mtu amnbaye atapata
jambo bila kulihitaji mwenyewe na kuondokana na dhana ya kutafutiwa kazi kama
wengi wanaofikiri.
Aliwataka wingi wao uwe
ni sehemu muhimu ya kutafakari muafaka wa Taifa la Tanzania ijao ikiwa ni
kushiriki katika ngazi mbalimbali za uongozi na kuondokana na dhana kuwa mwenye
uwezo wa fedha ndio sababu ya kushinda.
Mlezi huyo alisema
dhana ya fedha katika kutafuta uongozi ipo kwa baadhi ya watu kutokana na tabia ya
mtu mmoja mmoja lakini sio jambo la kusimamia kama kigezo.
Naibu Waziri aliwataka
vijana wa CCM kuondoa uoga katika maamuzi ambayo yanahusu maslahi ya Taifa na
jamii kwa ujumla iwapo sifa za uongozi unazo.
Makamba aliwaambia
vijana kutambua kuwa kiongozi wema wanatoka kwa mungu na kuachana na tabia ya
kulalamika kwakigezo kuwa nchi inaongozwa na wazee jambo ambalo wanalitengeneza
wenyewe.
Aidha aliwataka wasomi
kutafuta maandiko ambayo aliandika Hayati Mwalimu Nyerere kwani yana msingi
mkubwa katika kujitambua na kufanya maamuzi sahihi kuhusu nchi yao na uongozi
kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti Vyuo Vikuu Wilaya ya Dar es Salaam Abubakari
Asenga alisema katika mahafal;i hayo wanafunzi zaidi ya mmia nne kutoka vyuo 28
vya mkoa wa Dar es Salaam walishiriki katika sherehe hiyo.
Asenga alisema huo ni
uataratibu ambao wamekuwa nao tangu kuoanzishwa kwa shirikisho hilo lengo
likiwa ni kuwatambua na kuwapatia vyeti vya utambulisho wao ndani ya CCM.
Alitaja vyuo ambavyo
vilishiriki ni pamoja na Mwalimu Nyerere, Ustawi, Ardhi, UDSM, IFM, CBE, DIT,
TSJ na vingine vingi.
Kwa upande wa msoma
risala kwa niaba ya wahitimu Innocent Nsena alisema wanakiomba Chama Cha Mapinduzi CCM
kuwatumia wahitimu wanaomaliza vyuo kwani wana ujuzi na uwezo wa kukabiliana
na changamoto za jamii pamoja na vyama
vya upinzani hapa nchini.
Aidha alisema wanavyuo
wanapendekeza maoni yao kuhusu rasimu ya katiba ambapo wanaomba nchi ya
Tanzania kutokubali kuwa na serikali ya shirikisho kwani uwezo wa nchi bado ni
mdogo kuendesha nchi ambayo bado ni change kuichumi.
Pia wanapendekeza
upatikanaji mpya wa kupata mgombea urais ili kuondoa mpasuko ambao unatokea
mara kwa mara baada ya uchaguzi kufanyika.
Alisema katika
mazingira yoyote yale Rais bora lazima atokee CCM ila kutokana na mazingira mbalimbali
ambayo yamekuwa yakitokea baada ya uchaguzi ni vyema wakatumia mfumo wa kujaza
dodoso ili wana CCM wapendekeze Rais wanayemuhitaji kwa manufaa ya Taifa.
No comments:
Post a Comment