STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, June 8, 2013

Moyes, Wenger katika vita ya kumwania Fabregas

2013 cesc fabregas barcelona
KLABU ya Manchester United imeingia vitani dhidi ya mahasimu wao Arsenal baada ya kocha wake David Moyes kuweka bayana kwamba ipo tayari kumnyakua kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas anayewindwa pia kurejeshwa Emirates na klabu yake ya zamani.
Moyes, amenukulia akisema angependa kumsajili kiungo wa zamani wa Gunners ambaye hata hivuo majuzi aliweka bayana nia yake ya kuendelea kusalia kwa mabingwa wa Hispania, Barcelona.
Kiungo alikaririwa akisema angependa kusalia Nou Camp Nou ili kupigania namba yake licha ya kusajiliwa Mbrazili mwenye thamani ya Paundi Mil 50, Neymer.
Hata hivyo Moyes amesema atafanya kila njia kumnyakua mshindi huyo wa Kombe la Dunia aliyenyakua na timu yake ya taifa katika fainali zilizopita za 2010 ili kujenga kikosi chake.
Mipango ya Fabregas kurejeshwa Ligi Kuu ya England ilianza kitambo hata kabla Moyes kuchukua nafasi ya Ferguson mwzi uliopita.
Mabingwa hao wanamhitaji kiungo huyo baada ya Paul Scholes kustaafu na Michal Carrick kuondoka huku Tom Cleverley akibebeshwa majukumu yote.
Licha ya viungo toka Brazil, Anderson na Mjapan Shinji Kagawa kufanya vyema Old Trafford, lakini wanaelezwa sio wa daraja la Fabregas na ndiyo maana Moyes anamtolea macho akichuana na Wenger aliyetangaza kutaka kumrejesha nyota wake huyo wa zamani aliyemuuza mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment