STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, June 8, 2013

Moyes amnyakua kinda toka Uruguay

http://e2.365dm.com/13/06/660x350/Guillermo-Varela_2955853.jpg?20130607111408
Guillermo Varela
KOCHA mpya wa Manchester United, David Moyes ameanza kazi kwa kumsainisha beki la kulia kinda  kutoka Uruguay, Guillermo Varela.
Valera mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa katika majaribio kwa mahasimu wa United, Manchester City msimu uliopita anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Moyes tangu amrithi Sir Alex Ferguson.
Mabingwa hao wa England watalazimika kuilipa klabu inayoshikilia taji la Ligi Kuu ya Uruguay, Penarol kiasi cha Paundi Milioni 1 kwa ajili ya saini ya mchezaji huyo, japo uhamisho wake unaweza kufikia mpaka Paundi Mil 2.5.
Varela alinukuliwa na gazeti la The Sun akithibitisha suala la kuhamia kwake United akisema alikuwa afanyiwe vipimo hivyo jana kabla ya leo Jumamosi kujiunga na kikosi cha timu yake ya taifa ya vijana U20.
Pia mchezaji huyo alisema atajifunza Kiingereza ili aweze kumudu kuwasiliana na wenzake.
United imemnyakua mchezaji huyo kijana baada ya misimu michache kuwanyakua makinda wengine waliopo katika kikosi chake kutoka nchi za Amerika ya Kusini na Kati baada ya kuwavuta Javier Hernandes 'Chicharito', Angelo Henriquez na Wabrazil mapacha, Rafael na Fabio .
Duru za kimichezo zinasema tayari mchezaji huyo alishafanyiwa vipimo hivyo vya afya jana na hivyo kuwa rasmi mchezaji wa Old Trafford.

No comments:

Post a Comment