STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 28, 2013

TFF kuendesha kozi sita tofauti


Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.
Kozi hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Waamuzi wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka huu.
Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment