STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 28, 2013

Redd's Miss Vyuo Vikuu Tanzania 2013 kupatikana Julai 5

Mratibu wa shindano la Redd's Miss Vyuo Vikuu Tanzania, Agnes Mathew
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/09/Msanii-Ney-wa-Mitego-naye-akipagawisha-kwa-hisia-kali.jpg
Ney wa Mitego atakayenogesha shindano hilo Ijumaa ijayo
http://gushit.com/files/bookmark_photos/61d62d0476L.jpg
Rich Mavoko naye atakuwepo siku hiyo
JUMLA ya warembo 16 wanatarajiwa kuchuana kuwania taji la urembo la Redds Miss Vyuo Vikuu Tanzania 2013 linalotarajiwa kufanyika Ijumaa ijayo (Julai 5) kwenye ukumbi wa San Cirro, Sinza jijini Dar es Salaam.
Warembo hao wanatarajiwa kusindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa wasanii nyota nchini Ney wa Mitego, Rich Mavoko, Mori P, Rocka na madansa wengine.
Mratibu wa shindano hilo, Agnes Mathew wa kampuni ya Aggy Classic Entertainment alisema kuwa wasanii hao wawili ni baadhi ya watakaowasindikiza warembo 16 watakaochuana kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Shindano la Redd's Miss Vyuo Vikuu Tanzania 2013, litakalofanyika Julai 5 litasindikizwa na burudani toka kwa wakali kama Ney wa Mitego, Rich Mavoko, Rocka, Mori P na wengine," alisema.
Agnes alisema maandalizi ya shindano yao yanaendelea vyema na kuwataja baadhi ya warembo watakaochuana siku hiyo ambao kwa sasa wanaendelea kujifua mazoezini katika ukumbi wa Grand Villa, chini ya mkufunzi wao, Bless Ngowi kuwa ni Sia Mtui, Feube Urio na Rosemary Alloyce.
"Warembo wengine ni pamoja na Nyangeta Kiboja, Eveline Mathew, Juliet Msaki, Severine Minga," alisema Agnes.
Mratibu huyo aliongeza kwa kuwataja wadhamini  mbalimbali waliojitokeza kulipiga tafu shindano lake kuwa ni pamoja na Ngorongoro Coservetion, Redds, Lake gas, Cocacola, Cloud's Fm, Times Fm, Grand Villa Hotel, Sibuka Tv &Radio, EATV/Radio na Magic FM.
Agnes  alisema warembo watakaoshinda mchuano hiyo mbali na kujinyakulia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslim pia watapata nafasi ya kushiriki fainali za Redd's Miss Tanzania 2013 litakalofanyika baadaye mwaka huu na kutoa wito kwa mashabiki wa burudani kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo ambalo litakuwa na burudani nyingine mbali na muziki wa kizazi kipya kama njia ya kulinogesha zaidi.

Mwisho

No comments:

Post a Comment