STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 27, 2013

Hali ya Mzee Mandela bado tete

Mzee Mandela
BINTI wa Nelson Mandela anasema kiongozi huyo wa zamani wa Afrika kusini yupo katika hali mahututi.
Makaziwe Mandela alizungumza kwenye radio ya taifa Alhamis wakati wanafamilia walipokusanyika kwenye hospitali ya Pretoria Mediclinic Heart  ambapo Bwana Mandela amelazwa kwa siku ya 19 sasa.
Rais Jacob Zuma aliahirisha safari yake kuelekea Msumbiji Jumatano baada ya kumtembelea Mandela hospitali.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Barack Obama yupo nchini Senegal kwenye kituo chake cha kwanza katika ziara yake barani Afrika ya kuhamasisha biashara, uwekezaji na usalama wa chakula.
Ajenda zake alhamis zinajumuisha mikutano na dhifa rasmi ya chakula cha jioni na Rais wa Senegal Macky Sall pamoja na mazungumzo ya utawala wa sheria na viongozi wa mahakama katika eneo.
Bwana Obama na mke wake Michelle pia watatembelea kisiwa cha Goree, eneo la UNESCO World Heritage ambalo kutoka karne ya 15 hadi 19 lilikuwa kituo kikubwa cha biashara ya utumwa kwenye pwani ya Afrika.
Kutoka nchini Senegal, bwana Obama anapanga kuelekea Afrika kusini na kutembelea kisiwa cha Robben, gereza ambalo rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela alifungwa kwa takribani miongo miwili. Pia atasimama nchini Tanzania kabla ya kurejea nyumbani nchini Marekani. 
 
VOA

No comments:

Post a Comment