STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 27, 2013

Njemba yaua mtu kwa kisu, kisa...!

Na Esther Macha, Mbeya
JESHI la polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mkazi wa kijiji cha Saman’ombe wilayani Momba Mkoani hapa livingstone mulyatete (42) kwa kosa la kumuua kwa kumchoma kisu Patrick Yohana (30)baada ya marehemu kumtania mtuhumiwa kuwa amenunua piki piki mbovu.
Akizungumza na waandishi wa habari  Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani hapa Bw. Barakael Masaki alisema kuwa tukio hilo limetokea juni 26 mwaka huu majira ya saa 12.30 mchana katika kijiji cha Samang’ombe .
Bw. Barakael alisema kuwa chanzo cha ugomvi huo kati ya marehemu na mtuhumiwa ni ugomvi uliotokea kati yao baada ya marehemu kumtania mtuhumiwa kuwa piki piki yake ni mbovu ndipo alipochukua kisu na kumchoma katika ubavu wa kulia na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani mara moja na kujibu tuhuma hizo dhidi yake.
Aidha Kamanda Masaki ametoa wito kwa jamii kudhibiti hasira zao ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

No comments:

Post a Comment