STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 27, 2013

Brazil yatangulia fainali za Mabara, waisubiri Hispania au Italia

Delight: Fred celebrates his strike in front of the adoring fans in Belo Horizonte
Neymar na mchezaji mwenzake wakishangilia bao la Brazili jana

Response: Edinson Cavani equalised for Uruguay early in the second half
Edinson Cavani akishangilia bao lake la kusawazisha jana
WENYEJI wa michuano ya Kombe la Mabara, Brazil usiku wa kuamkia leo walitangulia Fainali za michuano hiyo baada ya kuisasambua Uruguay kwa mabao 2-1 katika pambano kali la nusu fainali.
Bao la  kichwa la dakika za 'jioni' lililofungwa na Paulinho liliivusha Brazil katika hatua hiyo na kusubiri mshindi wa mechi ya leo kati ya Hispania na Italia zitakazoumana katika nusu fainali ya pili.
Uruguay itajilaumu kwa kushindwa kuibuka na ushindi katika mechi hiyo baada ya kuanza kipindi cha kwanza na kupata penati iliyopotezwa na mshambuliaji wake, Diego Forlan kabla ya Brazil kujipatia bao la kuongoza dakika ya 41 kupitia Fred.
Bao hilo lililotokana na shuti kali la Neymer kusindikizwa wavuni na Fred lilidumu hadi wakati wa mapumziko.
Hata hivyo iliwachukua dakika tatu tu Uruguay kulirejesha bao hilo katika kipindi cha pili kilipoanza baada ya Edinson Cavani alipofunga bao baada ya kuiwahi pasi ya Thiago Silva na kufanya pambano kuwa gumu zaidi hadi dakika ya 86 Paulinho alipofunga bao hilo la ushindi.
Hiyo ni mechi ya nne mfululizo kwa Brazil kushinda ikiwa chini ya kocha Luiz Felipe Scolari katika michuano hiyo ambayo ni ya kuikaribisha fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyikia nchini humo mwakani.
Wakati Brazil ikiwa imeshatangulia kwenye fainali timu nyingine ya pili itakayopumana nayo itafahamika usiku wa leo wakati Hispania itakapoumana na Italia ambayo itawakosa nyota wake kadhaa akiwemo Mario Balotelli.
Pambano hilo la Italia na mabingwa wa Ulaya na Dunia, Hispania itakumbusha fainali za Euro 2012 timu hizo zilipokutana na Italia kucharazwa mabao 4-0.

No comments:

Post a Comment