STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 27, 2013

Kisura wa Miss Utalii ang'ara Kosovo, Bodi yampongeza


Mrembo Mwanakombo Kessy akipata kiburudisho baada ya kazi nzuri nchini Kosovo
Mwanakombo Kessy akiwa na warembo wenzake baada ya shindano la Miss Freedom of the World na kutwaa taji la Best Model


MSHINDI namba tano wa shindano la Miss Utalii Tanzania, Mwanakombo Kessy amefanikiwa kunyakua tuzo ya 'Mwanamitindo Bora' katika mashindano ya Miss Freedom of the World 2013 lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kosovo na Bodi ya Miss Utalii Tanzania imepongeza.
Mrembo huyo alishinda taji hilo Juni 24  na kuwa taji la sita la kimataifa kwa Tanzania kunyakua kupitia shindano la Miss Utalii.
Kwa ushindi huo kisura huyo amevuna mkataba mnono wenye thamani ya Sh Mil 64 na kampuni ya kimataifa ya Johns Jonson ya Massimo Buttiglieriom.
Kutokana na mafanikio hayo Bodi ya Miss Utalii imemmiminia pongezi kisura huyo na kufurahia kazi kubwa aliyoenda kuifanya Kosovo na kudai ni muendelezo wa rekodi nzuri la shindano lao anga za kimataifa.
Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo 'Chipps', alisema wamefurahi mno kwa tuzo aliyopewa Mwanakombo na wanampongeza kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuipeperusha vyema bendera ya tanzania na kuonyesha shindano lao sivyo linavyochukuliwa hapa nchini.
"Ushindi huu ni kwa Taifa zima la Tanzania, watanzania wote hata wale wabaya wetu, wapika majungu wetu, wazushi wetu na wazee wa fitina. Tunatambua ushindi huu wa taji la 6 la kidunia, na mafanikio yetu kila mwaka katika mashindano ya Dunia, " alisema Chipps.
Chipps alisema wanampongeza mrembo wao na wanamsubiri kwa hamu atakaporejea nchini kwa ajili ya kumpa mapongezi ya heshima kwa alichokifanya ikiwa ni siku chache baada ya kushika nafasi ya tano katika shindano lililofanyika jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment