Rais wa Marekani, Barrack Obama anayetarajiwa kutua nchini wiki ijayo |
TAMASHA
la Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha
wasanii Mwanzega Mkuranga limeahirishwa ili kutoa nafasi kwa wasanii na viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya Rais wa Marekani, Baraka Obama.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caaasim Taalib alisema jana
kuwa wanachama wengi waliokuwa washiriki tamasha hilo watakuwa katika
maandalizi ya ujio wa Rais Obama hivyo litafanyika mwezi Agosti baada ya
sikukuu ya Idd el Fitri.
Taalib
alisema anawaomba radhi wananchi wa Mkuranga, viongozi mbalimbali na
wasanii washiriki wa tamasha hilo waliokuwa wamejiandaa kuonesha vipaji
vyao katika tamasha hilo .
‘Tumeamua
kutoa nafasi hii kwa wanachama wa SHIWATA ili washiriki kikamilifu
kudumisha amani katika wakati huu ambao tunatembelewa na Rais Obama na
wasanii washiriki kikamilifu, tunaomba tutoe taarifa katika vyombo vya
dola mara tunapoona kuna unjifu wa amani’ alisema Taalib.
Mwenyekiti
huyo alisema mgeni rasmi aliyekuwa ameandaliwa, Naibu Waziri wa Kilimo,
Adam Malima amepelekewa ujumbe huo pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wabunge wa Dar es Salaam nao
wamearifiwa kuhusu kusogezwa mbele tamasha hilo .
Alisema
sambamba na tamasha hilo, SHIWATA ilikuwa ikabidhi nyumba kwa mchezaji
wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na
wasanii wengine 14 ambao wamekamilisha michango ya ujenzi wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.
Wengine
watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole Matovola
‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni wanachama wa SHIWATA wangine ni Mwandishi
wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la Magereza, Flora
Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpaka
sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika eneo la
hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili
kujikwamua kimaisha.
No comments:
Post a Comment