STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 27, 2013

Yanga kuanza kujifua kwa msimu mpya Julai 2


Kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu, Yanga
MABINGWA wa kandanda nchini, Yanga inatarajiwa kuanza kujifua kwa mazoezi Julai 2 kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na hasa pambano lao la Ngao ya Jamii dhidi ya Azam.
Mazoezi hayo yataanza baada ya wiki mbili za mapumziko walizopewa wachezaji na benchi zima la ufundi la klabu hiyo na yatafanyikia kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, Mabibo Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya mtandao wa klabu hiyo, wachezaji wote na benchi la ufundi wataanza mazoezi siku ya Jumanne Julai 02 majira ya saa 2 asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu inayotarajiwa kuanza rasmi Agosti 24 mwaka huu.
Taarifa hiyo inasema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ernie Brandts ambaye yupo kwao nchini Uholanzi kwa mapumziko ya wiki mbili, anatarajiwa kurejea nchini Julai Mosi na siku itakayofuata ataongoza mazoezi ya timu yao akishirikiana na kocha msaidizi, Fred Felix Minziro.
Yanga inaanza mazoezi mapema ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuhakikisha inatetea ubingwa wake na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, awali Yanga ilianza mazoezi june 3 kujianda na mashindano ya kombe la Kagame ambalo serikali ilizizuia timu za Tanzania kushiriki mashindano hayo kutokana na hofu ya usalama nchini Sudan.

No comments:

Post a Comment