STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 27, 2013

BFT yasisitiza uchaguzi wake upo palepale Julai 7

Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limesisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu wake uliopangwa kufanyika Julai 7 upo pale pale jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kuwa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika juzi chini ya Rais wao, Joan Minja kimeamua kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangawa licha ya kuwepo na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya wadau wa ngumi.
"BFT inasisisiza kuwa uchaguzi upo kama kawaida Julai 7 licha ya aliyewahi kuwa kiongozi kati ya wale waliojiuzulu kutokana na kashfa ya dawa za kulevya, Anakoly Godfrey kupotosha kwamba uchaguzi huo hautafanyika," alisema Mashaga.
Katibu huyo alisema fomu za uchaguzi huo zilianza kutolewa Juni 4 kwenye ofisi za BMT na jijini Mwanza na mwisho wa kuzirudisha ni Julai 4 na siku inayofuata itakuwa siku ya usaili.
"Julai 6 itakuwa siku ya kupitia mapingamizi na kutolea maamuzi na Julai 7 ni siku ya uchaguzi wa BFT kupata viongozi wapya baada ya uongozi wetu kumaliza muda wake tangu Aprili," alisema.
Mashaga alitoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi ili kuweza kupata nafasi ya kuiongoza BFT na kuanza maandalizi ya kuiandaa timu kwa ajili ya michuano ya Ndondi ya Afrika itakayofanyika Septemba nchini Mauritius.

No comments:

Post a Comment