MFANYABIASHARA
wa madini ya Tanzanite, Bw. Steven Alex, amepigwa risasi jana jioni na watu
wanaodhaniwa kuwa majambazi eneo la Pangani, jijini Arusha na kuporwa zaidi ya
sh. milioni 60.
Kwa mujibu wa mashuhuda
wa tukio hilo, walisema mfanyabiashara huyo alikuwa ndani ya gari lake akiwa
amepaki eneo la Pangani ili aweze kulipa madeni kwa watu waliokuwa wamemuuzia
madini.
Walisema
ndani ya gari hilo ambalo lilifungwa vioo, alikuwa na wenzake wawili ambapo
ghafla walitokea vijana watatu waliokuwa na pikipiki aina ya Toyo ambazo
namba zake hazikufahamika wakiwa wameifunika na mifuko ya nailoni.
“Walimgongea
dirishani wakitaka afungue mlango, huyu mfanyabiashara hakufungua ndipo vijana
hao walichomoa bastola na kuanza kugonga tena kwenye dirisha la gari.
Emmanuel Shilatu
No comments:
Post a Comment