Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage |
MWENYEKITI
wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, leo mchana amefanikisha upatikanaji wa
Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC), kwa wachezaji wawili wa klabu hiyo
kutoka nchini Burundi -Amissi Tambwe na Gilbert Kaze.
Wachezaji
hao wawili ambao pia ni tegemeo la timu ya soka ya taifa ya Burundi
(Intamba Murugamba), hawakucheza katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania
iliyochezwa jana kutokana na kutokamlika kwa uhamisho huo, jambo
lililoleta usumbufu mkubwa kwa benchi la ufundi, wachezaji wenyewe,
uongozi na wapenzi na washabiki wa klabu.
Rage
aliondoka jijini Dar es Salaam jana usiku na imechukua chini ya saa 24
kuweka kufanikisha suala hilo. Katika taarifa yake kwa wana Simba,
Mbunge huyo wa Tabora Mjini alisema amelazimika kuingilia kati suala
hilo kwa sababu lilihusu baadhi ya taratibu muhimu za Shirikisho la Soka
Duniani (FIFA) na ukweli kwamba viongozi wa Vitalo, klabu waliyotoka
wachezaji hao hawakuwa mjni na hivyo kuchelewa kwao kungeigharimu
Simba.
"Kila
walipokuwa wakipigiwa simu kwa takribani siku tatu mfululizo walikuwa
wakisema kwamba wako milimani. Sasa hawa watu wa Burundi wakikwambia
wako miliman wanamaanisha wameenda kijijini kwao. Kuongea kwa simu pekee
kusingetosha na ndiyo Kamati ya Utendaji ya Simba iliomba niende
mwenyewe Burundi ili suala hili liishe," alisema.
Hii
ni mara ya pili kwa Rage, ambaye ana uzoefu wa kuongoza soka kwa zaidi
ya miongo mitatu, kuingilia kati suala la uhamisho wa wachezaji wa
kimataifa. Miaka miwili iliyopita, Mwenyekiti huyo alilazimika pia
kusafiri kwenda nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kushughulikia uhamisho
wa mchezaji Gervais Kago ambao nao ulikuwa na matatizo.
Kutokana
na kupatikana kwa ITC hizo, Kaze na Tambwe sasa wataruhusiwa kucheza
katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya JKT OIljoro ya Arusha iliyopangwa
kufanyika Jumatano ijayo mjini Arusha. Klabu ya Simba tayari imewakatia
wachezaji hao vibali vya kufanya kazi hapa nchini.
Wachezaji
wengine wa kigeni wa Simba, Joeph Owino na Abel Dhaira, walicheza
katika mechi ya jana kutokana na kukamilisha taratibu zote za uhamisho
na kuwa na vibali vya kufanya kazi hapa nchini.
Imetolea na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
SimbaSC
No comments:
Post a Comment