RPC Mbeya, Diwani Athuman
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya limewaonya mashabiki wa soka mkoani humo ambao Jumamosi walifanya vurugu kubwa na kusababisha kuutia doa mkoa huo katika medani ya soka.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo mkoani humo limewaonya mashabiki hao kuwa kama watgaendelea kufanya 'upuuzi' wao kama walivyofanya katika pambano kati ya Mbeya City na Yanga basi watakiona cha moto.
Jeshi hilo limelaani vurugu hizo ikidai linauchafua mkoa wao na pia ni tishio kwa Mbeya kuweza kufungiwa na hivyo kuwanyima mashabiki wa kweli wa soka kushuhudia mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Taarifa rasmi ya jeshi hilo la Polisi iliyotiwa saini na ASP P Mhako kwa niaba ya RPC Diwani Athuman isome mwenyewe hapo chini;
--
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANAWATAKA MASHABIKI NA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU WAACHE VITENDO VYA
KUFANYA VURUGU KATIKA MICHEZO ITAKAYOKUWA IKIFANYIKA KATIKA UWANJA WA
KUMBUKUMBU YA SOKOINE NA MKOA KWA UJUMLA, KWANI VURUGU HIZO
ZITASABABISHA MICHEZO HIYO KUHAMISHIWA SEHEMU NYINGINE NA WAPENZI KUKOSA
BURUDANI PIA WANANCHI KUKOSA KIPATO, HIVYO KUUTANGAZA MKOA WETU
VIBAYA.
VURUGU
ZILIZOTOKEA JUMAMOSI TAREHE 14/09/2013 KWA MASHABIKI KULISHAMBULIA GARI
LA VIONGOZI WA TIMU YA YANGA LILILOKUWA LIMEPAKI NJE YA UWANJA PIA
KULISHAMBULIA KWA MAWE GARI LILILOKUWA LIMEBEBA WACHEZAJI WA TIMU YA
YANGA NA KUHARIBU KIOO CHA MLANGO WA DEREVA NA KUFANYA MAANDAMANO AMBAYO
YAMESABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA SI CHA
KIUNGWANA NA KISIJIRUDIE TENA KATIKA MICHEZO MINGINE.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA HAKURIDHISHWA NA VITENDO HIVYO NA KUWATAKA
MASHABIKI NA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU KUWABAINI NA KUWATAMBUA WALE
WOTE WATAKAOFANYA VURUGU NA KULIJULISHA JESHI LA POLISI.
AIDHA
JESHI LA POLISI HALITAVUMILIA VITENDO HIVYO NA KWA YEYOTE
ATAKAYE/WATAKAO BAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA ZIDI
YAKE/YAO.
Signed by:
[P.A MHAKO – ASP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment