STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 2, 2013

Promota wa Cheka na Mmarekani aachiwa kwa dhamana


Promota Jay Msangi (katikati) akiwa na Bondia Mmarekani (kushoto) aliyekuwa aje kupigana na Bondia Mtanzania, Alphonce Mchumiatumbo katika pambano hilo la juzi.
****************************************

PROMOTA aliyeandaa pambano la Kimataifa la ubingwa wa dunia la uzito wa super middle kati ya bondia Francis Cheka na bondia kutoka Marekani, Phil Williams, Jay Msangi wa kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion, aliyekuwa akishikiliwa na Polisi tuhuma za kumdhulumu bondia kutoka Marekani, ameachiwa nje kwa dhamana.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova, amenukuliwa jioni hii kuwa, promota huyo aliyekuwa amekamatwa juzi Jumamosi mchana maeneo ya Oysterbay kwa mahojiano na kulala ndani kwa saa 24 ameachiwa huku upelelezi juu ya tuhuma zake zikichunguzwa.

Kamanda Kova, alisema promota huyo alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kushindwa kumlipa Williams kiasi cha Dola za Kimarekani 8,200 walizokubaliana.
Kova ambaye ni Mlezi wa Ngumi nchini, alisema jambo lililofganywa na promota huyo linaweza kuitia doa Tanzania kimataifa na kusababisha watanzania kukosa kuangalia mipambano mikubwa kama iliyochezwa mwishoni mwa wiki kwa wachache wasiokuwa waaminifu.
Hata hivyo alisema jeshi la Polisi litaendelea kuchunguza kwa vile kinachoonekana ni kwamba bodnia huyo wa Marekani na promota huyo walikubaliana wenyewe hivyo watakacopfanya kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa ili kumfanya Mmarekani huyop kurejea kwao akiwa na amani.

Katika pambano hilo  Cheka alimchapa Williams kwa pointi na kutwaa ubingwa wa WBF, ambapo kabla ya mipambano hiyo mabondia kadhaa waliopangwa kupigana siuku hiyo waliogoma kwa muda kupanda ulingoni wakishinikiza walipwe fedha zao.

1 comment:

  1. http://www.worldboxingfoundation.com/champions/current-wbf-world-champions ingia hiyo link utaona hili pambano WBF hawalijui na wala Williams sie bingwa wa huo mkanda

    ReplyDelete