STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 18, 2013

Cameroon yaungana na Nigeria, Ivory Coast kutangulia Brazili WC 2014

Nahodha Et'oo akiwajibika uwanjani katika mechi ya jana ambapo Cameroon ilishinda mabao 4-1

 
Huku wawakilishi watatu wa Afrika kwenye fainali za FIFA za kombe la dunia wakiwa tayari wamefahamika,timu hizo ni NIgeria, Côte d'Ivoire na Cameroon , kuna dalili zote wawakilishi wa Bara hilo wakatoka ukanda wa Magharibi.
Ghana iliyoifumua Misri mabao 6-1 kesho itaavana na wapinzani wao hao wakiwa na dalili zote za kufuzu sawa na ilivyo kwa Burkina Faso watakaocheza na Algeria 3-2.
Sare zozote za ugenini kwa timu hizo za Afrika Magharibi dhidi ya Waarabu zitafanya wawakilishi wa Afrika kwa mwakani nchini Brazili kuwa za ukanda huo kama ilivyokuwa mwaka 2010 katika fainali za WOZA.
Nigeria ilianza kukata tiketi hiyo juzi kwa kuinyuka Ethiopia kwa mabao 2-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya mechi ya kwanza kushinda 2-1.
Mabao ya Victor Moses kwa penati na Victor Obinna yalitodha kuivusha Nigeria katiia fainali hizo, huku kocha wake, Stephen Keshi akiweka rekodi kuwa kocha wa kwanza Muafrika kuzipeleka timu mbili tofauti katika fainali hizo.
Keshi aliipeleka Togo katika fainali za mwaka 2006 nchini Ujerumani na safari hii akiwa na Nigeria, pia mwenyewe akishacheza fainali hizo wakati wa uchezaji wake.
Katika mechi nyingine ya mtoano wa bara la Afrika, Ivory Coast ililazimishwa sare y 1-1 na Segenal, lakini Tembo hao Afrika walifuzu kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya mechi ya kwanza wakiwa nyumbani kushinda mabao 3-1.
Segenal walitangulia kupata bao kupitia kwa Moussa Sow kabla ya Ivory kuepuka kipigo cha mara ya kwanza tangu kwa karibu mwaka na nusu sasa kwa kusawazisha kupitia kwa Salomon Kalou.
Jana Simba Wasiofugika, waliungana na Nigeria na Ivory Coast kutinga fainali hizo za Brazil baada ya kuizamisha Tunisia kwa mabao 4-1.
Mabao ya Cameroon yalifungwa na Pierre Webo, Benjamin Moudandjo na kiungo mkongwe Jean Makoun aliyefunga mabao mawili.

Katika pambano la kwanza timu hizo zilishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu ya kutofungana.

No comments:

Post a Comment