STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 4, 2013

Diego Costa azidi kuchana nyavu A. Madrid ikiifukuza Barca

Diego Costa celebrates for Atletico Madrid
Diego Costa akishangilia bao lake la jana dhidi hya Athletic Bilbao
MSHAMBULIAJI nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa ameendelea kudhihirisha ni moto wa kuotea mbali baada ya jana kufunga bao lake la 13 katika La Liga na kumkamata Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, huku akiisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao.
Costa aliyekuwa ameachwa na Ronaldo baada ya nyota huyoi wa Kireno kufunga mabao mawili wakati timu yake ikiifunga Rayo Vallecano, alifunga bao hilo katika dakika ya 41 likiwa ni la pili kwa Atletico Madrid baada ya awali David Villa kutangulia kufunga bao la kuongoza dakika ya 33.
Ushindi huo wa Atletico umeifanya timu hiyo kuendelea kuifukuza mabingwa watetezi, Barcelona waliopo juu yao katika msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti na pointi moja.
Barcelona yenywe ina pointi 34 na Atletico imekusanya pointi 33 timu zote zikiwa zimecheza michezo 12, nafasi ya tatu ikiwa inashikiliwa na Real Madrid yenye pointi 28.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo ya Hispania, Valencia ilipata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Getafe nayo Granada ilipata ushindi kama huo ugenini dhidi ya Levante naMalaga ikiwa nyumbani iliinyuka Real Betis kwa mabao 3-2. Leo katika ligi hiyo kuna mchezo mmoja tu kati ya Elche dhidi ya Villarreal.

No comments:

Post a Comment