STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 4, 2013

Kombe la Dunia kutua tena nchini

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgtYbw_PVUbcO_y9ZUz619vY3Dxe-PLUHAYUtbg8x3y3D2kWnWTEvxppaVj2MmA6Zy7h4v99re623LlokJlXKcD0CQqtsodC3_tcN5WDErf8x5XPBjxrP7VdMznSlJHIm3K8EpMlZgZYNw/s400/FIFA+World+cup+_trophy.jpg
KOMBE la Dunia ambalo litashindaniwa mwakani nchini Brazil, linatarajiwa kutua nchini mwishoni mwa mwezi huu na watanzania watapata fursa ya  kupiga nalo picha.
Kombe hilo litatatua nchini ikiwa ni mara ya tatu na kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo litatua Novemba 29-30 likitokea Kenya.
Ziara hiyo ya Kombe hilo la Dunia inadhaminiwa na kampuni ya Coca Cola na kwamba itahusisha nchi kadhaa na itaendelea hadi April kwa kutua Brazil tayari kwa kujiandaa na fainali za michuano hiyo zitakazofanyika nchini humo mwaka 2014.
Tanzania na Kenya ni nchi pekee za Ukanda wa afrika mashariki zilizobahatika kuwepo kwenye ratiba ya ziara ya Kombe hilo kwani baada ya kutoka Tanzania taji hilo linaloshikiliwa kwa sasa na Hispania litatua Afrika Kusini na kuendelea kwenye mataifa mengine.
Baadhi ya nchi za Afrika zilizobahatika kupangwa kulipokea Kombe hilo ni Misri, Algeria, Ghana, Morocco na Tunisia.

No comments:

Post a Comment