STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 4, 2013

Monaco yaonja kipigo cha kwanza, ikiiacha PSG itambe kileleni

Nolan Roux scores Lille's first against Monaco
Roux akiifungia Lille moja ya mabao yaliyoizima Monaco jana
MABAO mawili yaliyofungwa na Nolan Roux wa Lille yamezima mbio za Monaco kufukuzana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Ufaransa, PSG, baada ya kupata kipigo chao cha kwanza katika ligi hiyo msimu huu.
Monaco na PSG ndizo timu zilizokuwa zikichuana kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo zikiwa pekee hazijapoteza, lakini kipigo hicho cha mabao 2-0 toka kwa Lille limneifanya Monaco kuiacha PSG itambe pekee yake kwa sasa.
Roux alianza 'kuwatengua' udhu, Monaco dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza kwa bao lililotokana na kazi kubwa iliyofanywa na Basa na kudumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili pamoja na Monaco kucharuka na kuwakimbiza wenyeji wao kupitia mshambuliaji wake nyota Radamel Falcao, lakini walijikuta wakifungwa tena bao la pili na mshambuliaji huyo wa Kifaransa, Raux kwa mara nyingine katika dakika ya 71.
Kwa kipigo hicho Monaco imesaliwa na pointi 25 na kuiacha PSG iliyoshinda Ijumaa kwa mabao 4-0 dhidi ya Lorient itulie kileleni ikiwa na pointi 28 ikifuatiwa na Lille yenye pointi 26 baada ya kila timu kucheza mechi 12 mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment