STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 4, 2013

Prisons yafa nyumbani, duru la kwanza kufungwa wiki hii

Prisons Mbeya iliyolala jana Sokoine
Oljoro JKT iliyopifumua Prisons-Mbeya
WAKATI pazia la duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara likitarajiwa kufungwa wiki hii kwa michezo saba ya raundi 13 kuchezwa kwenye viwanja tofauti, Prisons ya Mbeya imeendelea kuwa urojo baada ya jana kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Oljoro JKT.
Prisons ambayo ilikuwa imetoka kupokea kipigo cha bao 2-0 toka kwa 'ndugu' zao Mbeya City, jana ilikubali kipigo hicho kingine na kuwafanya wazidi kuchechemea kwenyue ligi hiyo inayofikia ukingoni kwa mechi za duru la kwanza.
Bao pekee lililoizima wajelajela hao na kuisaidia Oljoro kupanda kutoka nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu hjadi nafasi ya 11 ikiishusha Ashanti United katika nafasi hiyo, lilifungwa na Amir Omary.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena keshokutwa kwa mechi nne ambapo maafande wa JKT Ruvu wanaouguza kipigo cha mabao 4-0 toka kwa Yanga itaikaribisha Coastal Union kwenye uwanja wa Chamazi, huku Simba na Ashanti United zikiumana kwenye uwanja wa Taifa na Ruvu Shooting itakuwa kwenye dimba lake la nyumbani Mabatini-Mlandizi kuikaribisha Mtibwa Sugar na Kagera Sugar ikiwa Kaitaba mjini Bukoba itaumana na wageni wao Mgambo JKT.
Mechi za kufungia rasmi pazia la ligi hiyo litafungwa Alhamisi kwa mechi tatu kati ya mabingwa watetezi Yanga itakayocheza na Oljoro JKT uwanja wa Taifa, Azam na Mbeya City zitamaliza ubishi baina yao kwenye uwanja wa Chamazi na Rhino Ranger itakuwa mjini Tabora kuikaribisha Prisons katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Baada ya mechi hizo timu zitaenda mapumziko kupisha maandalizi ya timu ya taifa kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza katikati ya mwezi huu, huku pia pazia la dirisha dogo la usajili likifunguliwa tayari kwa duru la pili litakaloanza mapema mwakani.

No comments:

Post a Comment