STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, November 29, 2013

Yanga yaifuata Coastal fainali za Uhai Cup


http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2013/09/Yanga.jpg

TIMU ya soka ya vijana ya Yanga, imeonyesha dhamira yao ya kunyakua taji la Uhai 2013 baada ya jioni hii kuinyuka Mtibwa mabao 3-1 katika pambano la Nusu Fainali ya michuano hiyo inayohusisha timu za U20.
Kwa ushindi huo umeifanya Yanga sasa kujiandaa kukutana na Coastal Union katika pambano la fainali litakalochezwa Jumapili ili kupata bingwa mpya baada ya Azam kuvuliwa taji hilo jana.
Yanga na Coastal zinakutana kwa mara ya pili kwani zilikuwa katika kundi moja na ilishuhudiwa Yanga ikiinyoa Coastal mabao 2-1, hivyo kulifanya pambano hilo la Jumapili kutarajiwa kuwa gumu.
Yanga ilipata ushindi huo katika mechi hiyo ya leo iliyochezwa kwenye uwanja wa Chamazi kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Notikel Masasi aliyefunga dakika ya 17 na 32, kuizima Mtibwa iliyotangulia kufunga bao dakika ya 14 kupitia Shiza Kichuya.
Bao lililoikatisha tamaa Mtibwa iliyoishangaza Simba kwa kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuifumua 3-2 na kutiha hatua hiyo lilifungwa dakika ya 86 na Hamis Issa.

No comments:

Post a Comment