STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, November 29, 2013

Sare ya Zimbabwe yaipaisha Tanzania viwango vya FIFA, Burundi haooo!

Taifa Stars ya Tanzania
TANZANIA imepanda nafasi tano zaidi katika viwango vya Fifa, hivyo sasa kuwa ya 124 kutoka 129 iliyokuwepo mwezi Oktoba, huku Zimbabwe waliotoka suluhu na Taifa Stars wiki iliyopita ikishuka kwa nafasi nne na sasa kuwa ya 106 toka 102.
Zambia ambayo jana ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kilimanjaro Stars ikiwa kama timu alikwa kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyoanza juzi jijini Nairobi, Kenya, imeshuka nafasi tano na sasa ni ya 72 katika viwango hivyo.
Katika nchi za Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Uganda ndiyo inayoshika nafasi ya juu ikiwa ya 86 duniani licha ya kushuka kwa nafasi moja mwezi huu.
Burundi ambayo imepanda kwa nafasi tisa, inashika nafasi ya pili kwa upande wa Cecafa ikiwa nafasi ya 112 duniani, ikifuatiwa na Kenya iliyopanda kwa nafasi moja na kuwa ya 117 duniani, huku Rwanda iliyopanda kwa nafasi mbili na kuwa ya 127, ikiburuza mkia kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Jirani zetu  DR Congo wanashika nafasi ya 84    baada ya kupanda kwa nafasi saba zaidi mwezi huu, huku kwa upande wa Afrika, Ivory Coast ikiongoza na kwa dunia ikishika nafasi ya 17.
Ghana iliyoshuka kwa nafasi moja, inashika nafasi ya pili kwa Afrika huku kwa dunia ikiwa ya 24 na kwa bara hili ikifuatiwa na Algeria iliyopo nafasi ya 26 duniani baada ya kupanda nafasi sita.
Hispania ndiyo kinara katika viwango hivyo ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina, Colombia, Ureno, Uruguay, Italia, Switzerland , Uholanzi, Brazil, Ubelgiji, Ugiriki na England ikiwa ya 13 baada ya kushuka kwa nafasi tatu mwezi huu.

No comments:

Post a Comment