STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, November 29, 2013

Coastal yatangulia fainali za Uhai Cup, Yanga Mtibwa leo Chamazi

http://4.bp.blogspot.com/-nA-VP6b8gcY/UM8Mq0GDQeI/AAAAAAAAJyY/QiHY76JM3rI/s1600/Uhai+Cup+Logo-1.jpg
TIMU ya vijana ya Coastal Union ya Tanga, jana ilifanikiwa kutangulia Fainali za u20 Uhai Cup baada ya kuwavua ubingwa Azam kwa kuinyuka bao 1-0. katika pambano la Nusu Fainali ya kwanza ya michuano hiyo inayochezwa kwenye uwanja wa Chamazi, neje kidogo ya Dar es Salaam.
Bao pekee la Wagosi wa Kaya jana lilifungwa na mshambuliaji Yussuf Chipo dakika ya 32 na sasa timu hiyo ya Tanga inasubiri mshindi kati ya Yanga SC, na Mtibwa Sugar mechi inayochezwa leo kwenye nusu fainali ya pili.
Ushindi huo wa Coastal ni muendelezo wa ubabe wake kwa Azam kwani katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya mwaka huu, waliishinda mabao 2-1 na kulipa kisasi cha kulazwa katika fainali zilizopita ambapo Azam walitwaa taji hilo.
Coastal sasa inasubiri kujua itacheza na ni siku ya Jumapili kati ya Yanga au Mtibwa ambazo zitaumana jioni ya leo.
Yanga ilitinga Nusu Fainali juzi baada ya kuichapa Ashanti United kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa  kwenye Uwanja wa Azam Complex, huku Mtibwa ikiizima Simba kwa mabao 3-2.

No comments:

Post a Comment