Mchezo umeisha! Bondia Ondrej Pala akiwa ameegemea kamba kujiepusha na kipigo zaidi kwa Dereck Chisora raundi ya tatu katika pambano la ngumi uzito wa juu lililofanyika kwenye ukumbi wa Copper Box Arena, London, Uingereza usiku wa kuamkia leo. Chisora alikuwa anatetea taji lake la WBO Intercontinental wakati taji la WBA International lilihusishwa pia.

Ondrej
Pala wa Jamhuri ya Czech alipambana hadi raundi ya tatu aliposalimu
amri kwa Knockout (KO), hilo linakuwa pambano la nne mwaka huu Chisora
kushinda, likiwemo lile la ubingwa wa Ulaya alilotwaa September kwa kumpiga Edmund Gerber raundi ya pili.

Dereck Chisora akimuadhibu mpinzani


Dereck Chisora naye alipokea mikono kadhaa ya mpinzani kutoka Czech

Dereck Chisora na promota Frank Warren (kulia) wakifurahia mafanikio ya mwaka 2013
No comments:
Post a Comment