STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 20, 2013

Hatimaye Okwii huyooo Jangwani, FIFA yabariki uhamisho wake Yanga

Hayaa sasa mmemuona  Okwii kama Bin Kleb anasema hivyo wakati Emmanuel Okwi alipotuia nchini jana.
Umati uliojitokeza klabuni jana
Akiwapungia mkono mashabiki kuwasalimu
Msafara
Emmanuel Okwi akilakiwa na shabiki maarufu wa Yanga, Steven (kulia) katika uwanja wa ndege wa Taifa wa Mwalimu JK Nyerere muda mfupi baada ya kufika.
Kama kawa Namba 25

Mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda aliyesajiliwa na Yanga SC, Emmanuel Okwi, ametua jijini Dar es Salaam akitokea nchini Uganda.

Mamia ya mashabiki wa Yanga walihudhuria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar kumpokea mwanasoka huyo mahiri aliyewahi kuichezea timu ya Simba SC.

Okwi ametua kwa ndege ya Shirika la Rwanda Air majira ya saa 10 jioni na kupokelewa na nyomi ya mashabiki wa Yanga pamoja na viongozi wa timu hiyo walioondoka naye.

Okwi anatarajiwa kuungana na kikosi cha Jangwani kitakachokwaana na mahasimu wao Simba SC katika mechi ya 'Nani Mtani Jembe' Jumamosi Desemba 21 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mechi ya mwisho ya watani hao wa jadi ilimalizika kwa sare ya 3 - 3 ambapo Yanga walitangulia kufunga na Simba wakasawazisha. 
Mchezaji huyo amesema atua Jangwani kufanya kazi na kwamba suala la usajili wake hapendi kuzungumzia kwani siyo jukumu lake, ingawa taarifa zinadai kuwa FIFA imetoa baraka zote Okwi kukipiga Yanga kutokana na uhamisho wake kuwa halali.


Ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati Okwi akiwasili jijini Dar akitokea Uganda kuungana na Yanga.

No comments:

Post a Comment