STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 20, 2013

Extra Bongo yadai haijamchukua Muumin jumla

Muumin akiwa na wanamuziki wa Extra Bongo wakifanya mazoezi
UONGOZI wa bendi ya Extra Bongo umesema kutua kwa muimbaji nyota wa muziki wa dansi nchini, Mwinjuma Muumin haina maana kwamba ina mipango ya kumnyakua mwanamuziki huyo.
Muumin ameungana na Extra Bongo kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na maonyesho ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya yatakayofanyika jijini Dar na mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki aliiambia MICHARAZO kuwa, Muumin ameungana nao tu kwa ajili ya maonyesho hayo yatakayowakumbushia mashabiki wa dansi 'Mafahali Watatu' waliotikisa nchini.
Choki alisema, Muumin ni mwanamuziki mkubwa nchini hivyo ni lazima mtu ujipange kuweza kummiliki ndiyo maana mpango wa kumchukua jumla haupo zaidi ya kufanya kazi kwa pamoja tu kwa maonyesho hayo ambayo kwa jijini Dar es Salaam wameongezwa ratiba kwa kufanyika mara mbili badala ya moja.
"Tunaye tu katika maonyesho hayo maalum ya sikukuu siyo kama tumemchukua jumla," alisema Choki.
Kuhusu ratiba ya maonyesho hayo maalum, Choki alisema Mkesha wa Krismasi sasa watafanya onyesho Meeda Club-Sinza jijini Dar es Salaam na siku ya Krismasi itakuwa Chikaz Pub kabla ya kuanza safari kuelekea Geita kuzindua ukumbi mpya wa Omega Splended Resort katika mkesha wa Mwaka Mpya na kufanya onyesho jingine nmoja kabla ya kwenda Kahama Januari 2 na baadaye mjini Bukoba. Baadaya hapo watarejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na uzinduzi wa albamu mbili kwa mpigo.

No comments:

Post a Comment