STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 20, 2013

Mtikisiko! Dk Nchimbi, Nahodha waenda na maji

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/01/dk-emmanuel-nchimbi.jpg
Dk Nchimbi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjt-ne_CSUlNifDQfpRrKmkJnGAblGUETzOSqn0C7rEPhXRO4emCsc60KCLEC8lXvloKL4kWLKjmncyikZloTncdA6A6VrbmON8awmQd5FdiUN3ODbINfbq0a3qOVDrkLWzOOljiCjUp-w/s1600/1.JPG
Dk Mathayo

http://kifltd.files.wordpress.com/2012/01/shamsi-vuai-nahodha.jpg
Mhe Shamsa Vuai Nahodha

MAWAZIRI wanne akiwamo Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel  Nchimbi, na yule wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe Shamsi Vuai Nahodha wameenguliwa kwenye wadhaifa wao baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bungeni zinasema kuwa waziri mwingine aliyetenguliwa wadhifa wake ni Dk Mathayo David Mathayo anayehusika na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo.
Kung'olewa kwa mawaziri hao waliohuishwa na Operesheni Tokomeza Ujangili nchini imefanya idadi ya mawaziri wa serikali ya awamu ya nne kung'oka madarakani kuwa wanne baada ya Balozi Dk Kagasheki kutangaza kujiuzulu mwenyewe, japo naye ni miongoni mwa waliotangazwa kutenguliwa cheo chake hicho.
Kabla ya hatua hiyo waziri Mkuu, Pinda alikuwa hatarini kung'olewa madarakani kama msimamizi mkuu wa serikali bungeni kutokana na sakata lililotia simanzi taifa licha ya kuwa na lengo zuri la kulinda hifadhi na maliasilia dhidi ya wavamizi, lakini alilieleza Bunge kuwa aliwasiliana na Rais Jakaya Kikwete na kumueleza kutengua nafasi za mawaziri hao.

No comments:

Post a Comment