STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 20, 2013

Kaseba, Alibaba kupima uzito kesho Friends Corner

https://thumbp4-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AO9WimIAAAeTUrQhBAAAACuEw6I&midoffset=2_0_0_1_1165878&partid=2&f=1214&fid=Inbox&w=3000&h=3000
Alibaba Ramadhani
https://thumbp4-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AO9WimIAAAeTUrQhBAAAACuEw6I&midoffset=2_0_0_1_1165878&partid=3&f=1214&fid=Inbox&w=3000&h=3000
Zumba Kukwe

https://thumbp4-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AO9WimIAAAeTUrQhBAAAACuEw6I&midoffset=2_0_0_1_1165878&partid=4&f=1214&fid=Inbox&w=3000&h=3000
Japhet Kaseba


MABONDIA Japhet Kaseba 'Champion' wa Dar es Salaam na Alibaba Ramadhan wa Arusha wanatarajiwa kupima afya na uzito kesho jumamosi saa nne asubuhi katika ukumbi wa friends corner hotel ambapo ndipo hapohapo pambano lao litafanyikia siku inayofuata ya jumapili tarehe 22/12/2013 kuanzia saa kumi jioni

Pambano hilo liloandaliwa na Ibrahim kamwe chini ya BigRight promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi likiwemo la ubingwa wa mkoa kati ya Karage Suba na bondia mkali anaechipukia kwa nguvu  Fadhili Awadh 'Tiger'  katika uzito wa wealter[66kgs] pambano la raundi kumi, nao wanategemea kupima hiyo kesho

Akizungumza na vyombo vya habari mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe alisema zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa  mabondia wanaotegemea kupima ni Mbarouk Heri atakayezipiga na Lusekelo Daudi, Issa Omar 'Nampepeche' na Hassan Kiwale ’Moro Best’, Zumba Kukwe na Jacob Maganga, Adam Yahaya na Harman Shekivuli, Jocky Hamis na Mbena Rajab, Ernest Bujiku na Shah Kassim, Shaaban Body-Kitongoji na Mwinyi Mzengela, Shaaban Manjoly na Kassim Chuma.

Nae Mtanzania aishie Canada Kareem Kutch atapigana na Tata boy kwa ajili ya pambano la kimataifa la mchezo wa kickboxing la raund tano, Mabondia wote wameshawasili Dar es salaam, wakati Alibaba Ramadhan wa Arusha na Jacob Maganga wa Tanga wamefikia katika hotel ya Valley View wakati Kutch yupo Durban Hotel Kariakoo wapo vema na wenye furaha kwa mapambano yao.

No comments:

Post a Comment