STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 20, 2013

Golden Bush Veterani kuendelea kutoa dozi kwa wazee wenzao?


WAKALI wa soka la veterani, Golden Bush Veterani wikiendi hii watakuwa na kibarua cha kuendelea kutoa 'dozi' kwa wazee wenzao katika michezo inayotarajiwa kuchezwa  Dar es Salaam.
Ifuatayo ni ratiba kamili ya mechi hizo kama ilivyotolewa na msemaji wao Onesmo Waziri 'Ticotico'.
 
Wadua,
 
Hii ndio ratiba kamili ya game ambazo Golden Bush tutacheza weekend hii na ile inayofuata.
 
Tarehe
Muda
Mechi No
Uwanja
mechi Na
21/12/2013
0800am
564U
Staki Shali
Staki shari Veterans
22/12/2013
0430pm
565H
Nagwanda Sijaona a k a TP
Kilwa Veterans
28/12/2013
0430pm
566U
Nagwanda Sijaona a k a TP
Wahenga Veterans
 
Niseme wazi kwamba timu yetu iko kwenye maandilizi ya mwishomwisho kabisa kabla ya kuumana na watani wetu wa jadi, Wahenga Veterans, hii itakuwa na game number 566U itakayopigwa uwanja wa TP Tandale alimaarufu Nangwanda sijaona. Itakumbukwa kwamba mwaka jana mechi kama hii wenzetu walishinda kwa goli za jioni sana, kwakutambua hilo walimu wetu akina Madaraka Selemani wamefanya kazi ya ziada kwa kurekebisha baadhi makosa na vilevile kucheza mechi nyingi sana za kirafiki ikiwa ni pamoja na kuvuka maji hadi visiwani tulipowapiga KMKM 2-1.
 
Timu iko sawasawa kutoa burudani kwa wapenzi wetu karibuni sana.
 
Pamoja na maandilizi hayo tunapenda kuwafahamisha kwamba Golden Bush tumemchukua bwana Jonas Afumwisye kuwa bounsa wetu hasa pale tunapocheza game nzito hasa zenye upinzani kama Wahenga.
 
Asanteni
Onesmo

No comments:

Post a Comment