STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 20, 2013

Breaking Newzz! Waziri Kagasheki ajiuzulu, kisa Operesheni Tokomeza

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2012/08/picha-no.-31.jpg
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Khamis Kagasheki amejiuzulu wadhifa wake huo.
Habari hizo zinasema sababu za kujiuzulu kwa Dk Kagasheki imetokana na mjadala mkali ulioendeshwa leo bungeni juu ya ripoti ya Tume ya kuchunguza kadhai ya OT (Operesheni Tokomeza) iliyohusisha kuwatoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi za Taifa na kuelezwa kuleta unyanyasaji na maafa makubwa wa wahusika kulikofanywa na waliondesha operesheni hiyo ambayo ilikuja kusitishwa.
Hata hivyo tunaendelea kufuatia juu ya taarifa hii, ingawa inadaiwa kuwa sababu za kujiuzulu kwa waziri huyo ni kutaka kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zilizotolewa katika uendeshaji wa operesheni hiyo.
Kujiuzulu kwako kunakaribia kufanana na kilichowahi kufanywa na Alhaji Ali Hassani Mwinyi wakati akiwa waziri wa Mambo ya Ndani kutokana na mauaji yaliyofanywa na polisi mkoani Shinyanga mwaka 1978.

No comments:

Post a Comment