STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 30, 2014

Fainali CHAN 2014 ni Ghana v LIbya, Nigeria kuwania mshindi wa tatu

Add caption
BLACK Stars ya Ghana usiku wa kuamkia leo iliifuata Libya iliyokuwa imetangulia hatua ya fainali baada ya kuichapa kwa mikwaju ya penati mahasimu wao, Nigeria katika pambano la nusu fainali lililokuwa kali na la kusisimua.
Ghana ilipenya hatua hiyo baada ya kumaliza dakika 120 na wapinzani wao wakiwa nguvu sawa kwa kutofungana kabla ya kuishinda kwa mikwaju ya penati 4-2.
Pamoja na kucheza pungufu kwa kumpoteza beki wake Adusei baada ya kuonyeshwa kati ya pili ya njano na kuunganishiwa nyekundu, lakini iligangamala na kuibana Nigeria ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa wapya wa CHAN-2014.
Baada ya dakika 90 kumalizika Ghana wakipwa pungufu na kuongezwa dakika 30 Black Stars walikomaa mpaka hatua ya matuta ambayo ilishuhudiwa vijana wa Stephen Keshi wakipachika mkwaju mmoja kati ya penati tatu walizopiga, mbili zikishindwa kuingia kimiani.
Wafungaji wa penati za Ghana walikuwa Akuffu, Anobaah, Ainooson na Attobrah, huku ile ya Super Eagles ikifungwa na Uzoenyi na zile za Kwambe na Uzochukwu zikikosa macho.
Kwa matokeo hayo Ghana itakwaruzana na Libya usiku wa Jumamosi, na Nigeria itapepetana na Zimbabwe katika pambano la jioni ya siku hiyo na kufungwa pazia la michuano hiyo ambayo taji halina mwenyewe baada ya Tunisia kukwama kwenda Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment