STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 30, 2014

Mbwana Samatta Mchezaji Bora wa TP Mazembe 2013


Samatta akiokota mpira nyavuni baada ya kutupia
MSHAMBULIAJI Nyota wa Kimataifa wa Tanzania anayeichezea TP Mazembe, Mbwana Samata, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2013 wa klabu hiyo ya DR Congo.
Mbwana alipata kura nyingi zaidi, kuwashinda wenzake, ambao kwa mujibu wa tovuti ya TP Mazembe, yeye alipata pointi 248, huku nafasi ya pili ikishikwa na Asante Solomon aliepata kura 219.
Ulikuwa ni mwaka wa mafanikio pia kwake, pia akiwa na kumbukumbu ya kutajwa kati ya wachezaji ambao wanawania tuzo za Wachezaji wanaocheza barani Afrika, nakuchujwa baadae.
Zaidi ya hiyo, ameisaidia timu yake ya TP Mazembe katika michuano ya ndani na kimataifa, bila kusahau msaada pia aliuutoa kwa timu yake ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

No comments:

Post a Comment