STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 30, 2014

Mhe. Temba, Cassim Mganga wana Lavalava la pamoja

Mhe Temba

Cassim Mganga

WASANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Mheshimiwa Temba na Cassim wanatarajia kuachia hadharani kazi yao mpya ya pamoja iitwayo 'Lavalava' Ijumaa wiki hii.
Akizungumza na MICHARAZO, meneja wa wasanii hao Said Fella, alisema wimbo huo umerekodiwa katika studio za Burn Records chini ya prodyuza Sheddy Clever.
Fella alisema 'kolabo' hiyo ni mwanzo tu kwa wasanii hao kutoka TMK Wanaume Family na ukoo wa Tip Top Connections kufanya kazi kwa pamoja ikiwamo kuja kuzalisha albamu kamili.
"Katika kuendelea udugu baina ya wasanii mbalimbali nchini, Mhe. Temba na Cassim Mganga wametengeneza wimbo wa pamoja uitwao 'Lavalava' na utaachiwa hewani kuanzia Ijumaa ijayo na kama mambo yakienda vyema wasanii hao wanaweza kuja kutoa albamu ya pamoja," alisema Fella.
Cassim anayefahamika kama 'Tajiri wa Mapenzi' anatamba kwa sasa na wimbo wake uitwao  I Love You', huku Mhe Tamba anakimbiza kupitia kibao chake kiitwacho 'Toroka Uje' alichoimba na Dogo Aslay na akiwa mbioni kuachia dokomentari yake iitwayo 'Maskini Jeuri'.

No comments:

Post a Comment