STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 30, 2014

Shaa abadili Sifa Ujinga kwa Subira

WIMBO mpya wa mwanadada Sarah Kais 'Shaa' unaofahamika kwa jina la 'Sifa Ujinga' unatarajiwa kuachiwa hadharani mwezi ujao ukiwa umebadilishwa jina na kuitwa 'Subira'.
Mmoja wa mabosi wa msanii huyo, Said Fella 'Mkubwa' aliliambia MICHARAZO kuwa, wadau waliousikiliza wimbo huo ndiyo waliotoa mapendekezo ya kubadilishwa kwa jina ili kuweza kuwa na mvuto kwa wasikilizaji.
Fella alisema kwa sasa wanafanya mipango ya kukamilisha video ya wimbo huo wa pili kwa Shaa chini ya lebo ya Mkubwa na Wanae aliyoingia nayo mkataba wa miezi sita ili kazi hiyo iachiwe rasmi mwishoni mwa Februari.
"Wimbo wa Shaa uitwao 'Sifa Ujinga' utaachiwa mwezi ujao lakini ukiwa na jina jipya la 'Subira' baada ya wadau wetu kuusikiliza na kupendekeza jina hilo jipya ambalo nasi tumeliafiki," alisema.
Shaa, nyota wa zamani wa Coca Cola Pop Star akishinda nchini na kuunda kundi moja na wasanii wenzake Witness na marehemu Langa na kuliita Wakilisha alitaoa 'Sugua Gaga' chini ya lebo hiyo Mkubwa na Wanawe.
Kabla ya hapo staa huyo wa nyimbo kadhaa ukiwamo wa 'Promise' alikuwa akifanya kazi chini ya umeneja wa prodyuza mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joacqim Kimario 'Master J'.

No comments:

Post a Comment